Wednesday 29 January 2014

Matatu Sticker jokes / quotes.

 

 Well Kenyan matatu's are known for their rather rude but wise sticker quotes/jokes. Here are some of them, feel free to add more:


  1. Usilete stress kwa gari.
  2. Usifungue madirisha, ungetaka upepo ungebebwa na bodaboda.
  3. Kama una haraka ungesafiri jana.
  4. Hakuna stage ya kumi,kula ndizi kisha ganda kalia uteleze mpaka tao
  5. Kama una haraka sana shuka ukimbie
  6. Songea mwenzako starehe ni kwa wheelchair
  7. Wauliza konda, iko kiti? Kwani wengine wamekalia ndoo
  8. Kulipa ni lazima Change ni ukikumbuka
  9. Dere ana bibi,konda anatafuta
  10. Kulipa fare kwa mwanaume ni kawaida lakini msupa tunaeza ongea
  11. Marehemu alituacha kwa kukosa kufunga mshipi kama wewe
  12. Unajifanya mkali kwa gari na kwako wewe ni bubu
  13. Ungesikiza mwalimu ukiwa shule saizi ungekua na gari yako
  14. Derefa ni yesu makanga ni saitani
  15. Hatusemi wewe ni mnono lakini ukikalia viti mbili ..
  16. Kushuta ni sare, kutapika soo
  17. Kupanda ni popote kushuka ni stage
  18. Kama inzi angeacha ujinga,angetengeneza asali 
  19. Ati mwisho wa gari ni hapo, Kwani ikipita hapo inakuwa ndege
  20. Ukiona fare iko juu ndiyo mwanzo wa msoto shuka ukimbize barabara
  21. Salimia huyo ako kando, kukatiana ni mkishuka!
  22. Msongee kidogo dere anashuka pale mbele uketi
  23. Hata ukipimwa sitaki!
  24. If you miss the driver, kiss the conductor
  25. Heri kununua MATATU kuliko kuoa BIBI Mkorofi!
  26. Ati hakuna kiti? Kwani hawa wako hapa wamekalia mikembe ya rangi
  27. Hata maji chafu huzima moto
  28. Kama gari iko na joto ,shuka upande fridge
  29. Nyamba ukitoka
  30. Kama hujanunua hapa usikulie hapa
  31. Ukichengwa tulia!
  32.  KARAO ALIPE GARI
  33. mbuzi kala mkeka,wadaku mtaketi wapi?
  34. Dere ni waya,konda ni faya..we huwesmek!
  35. Hakuna stage ya hapo dere. 
  36. Hata ukipimwa hakuna dawa
  37. Starehe ya gari ni kupanda nyuma.
  38. Dere ako sawa, konda fitty kabisa mbona wewe ni sumbua?
  39. Mapenzi kwa gari ni wanne wanne ka orbit!
  40. Unaringa na haujapimwa
  41. Dere ni moto, Konda ni wazimu, usituletee stress kwa hii gari!
  42. If the music is too loud then you are too old
  43. Unajifanya ngombe ukamuliwe na nani?
  44. Mzee ni wewe!
  45. Ukitaka kuketi starehe,nunua gari yako! 
  46. Unajifanya asali ulambwe na nani?
  47. Si ati ni gari haina mbio ,jam ndiyo kubwa
  48. Makosa ya marehemu ni kuwa hakutumia juala.
  49. Kama utamu waua,sumu ya nini?
  50. Usiharakishe dere...wee ndio umechelewa
  51. Mdomo mkubwa chapati waikunjia nini?
  52. More seat upstairs
  53. Usitoe viatu kwa gari!
  54. No calls please sms only
  55. Juzi sare,,
    Jana sare,,
    Acha aibu.!
    Lipa leo!

No comments:

Post a Comment